Mikoa ya Mtwara na Lindi sasa imeandika historia mpya baada ya kuzinduliwa kwa mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati nne na kufanya kituo cha Mtwara kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 22 kutoka megawati 18.
Mitambo hiyo iliwashwa jana Ijumaa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani saa 5:20 asubuhi katika kituo cha Mtwara kinachohudumia mikoa ya Lindi na Mtwara. mitambo hiyo imegharimu kiasi cha Sh bilioni 8.5 na hivyo kuongeza wigo mpana katika sekta ya uwekezaji katika miradi inayohitaji umeme.
Akizungumza katika hafla ya kuwasha mitambo hiyo, Dkt Medard Kalemani amesema kutokana na mikoa ya Lindi na Mtwara kukuwa kiuchumi tayari wameanza utaratibu wa kuagiza mitambo mingine miwili ili kufanya kituo cha Mtwara kuzalisha megawati 26 na kuwa na ziada ya umeme lakini kuvutia zaidi wawekezaji hasa wanaohitaji umeme wa uhakika.
“Tulichokifanya leo, hizi mashine mbili mpya, tumeziingiza kwenye gridi ya Taifa na kuongeza megawati nne, na kufanya kuwa na jumla ya megawati 22. Kwa sasa mahitaji ya mikoa ya Lindi na Mtwara ni takribani megawati 16 na hivyo tutakuwa na ziada ya megawati sita,”mesema Waziri.
Kupata habari kwa undani pamoja na picha Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.