Mkuu Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Muungano Waryuba amelitaka shilika la Viwango Tanzania (TBS) kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora katika uzalishaji wa bidhaa hasa vyakula. Amesema wananchi wanazalisha kwa kiwango chao cha uelewa wao hivyo shirika linapaswa kuwapa msaada wa kitaalam.
Kaulli hiyo ameitoa wakati wa ukaguzi wa mabanda ya wafanyabishara na wajasiliamli wadogo kwenye maeonesho ya Nanenane yanayoendelea uwanja wa Ngongo Liandi.
“Nitowe wito kwa TBS wajipambanue na kuwa na wigo mpana ambao utawawezesha kuwafikia wazalishaji wa bidhaa hizo ili zinapoingia sokoni zisiwe na madhara kwa watuamiaji.
Mhe Walyuba aliyekuwa Mgeni Rasmi wa maonesho haya amesema hatari ya madhara kwa mtu aliyetumia bidhaa isiyo kidhi viwango ni kubwa hivyo haitakiwi kuachwa kimyakimya”
Amesema amepitia mabanda mengi ambapo amekutana na changamoto hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.