Mganga Mkuu Mkoa wa Mtwara Dkt. Benedicto Ngaiza mapema leo hii ameongoza shughuli ya mapokezi ya Madaktari bingwa 64 wa Dkt. Samia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Katika mapokezi hayo Dkt. Ngaiza amesema Madaktari hao bingwa watatoa huduma za kimatibabu katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Mtwara na Hivyo kuwataka wananchi wote wenye shida mbali mbali kujitokeza kwa ajili ya kupata huduma hizo za kitabibu.
Dkt. Ngaiza akaongeza kuwa huduma hizo za kitabibu zitatolewa kwa wananchi wote katika vituo husika katika Halmashauri kwa muda wa siku sita kuanzia leo septemba 16, 2024 hadi septemba 22, 2024.
Katika Kutamatisha hotuba yake fupi Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Ngaiza akasema huduma zitakazotolewa na madaktari hao ni pamoja na Huduma bingwa za magonjwa ya wanawake na Ukunga, Huduma bingwa za Watoto na Watoto wachanga, Huduma bingwa za upasuaji wa mfumo wa mkojo, Huduma bingwa za magonjwa ya ndani, Huduma bingwa za Usingizi na Ganzi, Huduma bingwa za kinywa na meno, Huduma bingwa za wauguzi pamoja na Huduma bingwa za mifupa.
Septemba 16, 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.