Leo Juni 15,2024 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amemuapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Nanyumbu Mh. Christopher Magala ambae ameteuliwa juni 11, 2024.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Saluhu Hassan kwa kumteua Magala kuja kuendeleza majukumu katika Wilaya ya Nanyumbu pia amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuleta fedha za miradi inayoendelea kutekelezwa.
"Wananchi wa Nanyumbu wanatarajia kuona maendeleo makubwa yakitokea chini ya uongozi wako, wanategemea kuwa wewe msemaji wao, wanategemea hali ya utulivu na amani ambao wewe utasimamia, wanategemea kero na changamoto za kiuchumi kupitia wewe utaziondoa, kawasikilize wananchi wa Nanyumbu" amesema Kanali Sawala.
Amemtaka pia kusimamia hali ya ulinzi na usalama hususani eneo la mpakani kwani bila amani na utulivu hakuna maendeleo hivyo amemtaka kushirikiana na watu wa ulinzi na usalama.
Pamoja na hayo Kanali Sawala amemuagiza kusimamia miradi yote ya kimaendeleo na ahakikishe miradi yote inakamilika kwa wakati.
Kuchukua hatua kwa wale wote walioanzisha kero na kuangalia mfumo wa utendaji ili kutozalisha kero.
Kusimamia wakulima wa nanyumbu na kupata haki zao na viongozi wa amcos kutokuwa na janja janja za kula jasho la mkulima kwani karibia asilimia 85 ya wakazi wa Nanyumbu ni wakulima.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mh. Christopher Magala Amemshukuru Mkuu wa mkoa kwa kumpokea na kumuapisha na amemuahidi kuwa atasimamia katiba kanuni na miongozo inayotolewa na serikali ili aweze kutekeleza shughuli za maendeleo kwenye maeneo husika.
Pia ameahidi kutenda kazi kwa haki, kuzingatia maslahi ya watu, katiba na miongozo kusimamia miradi ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi kwa ujumla na kusimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ).
Aidha Mhe. Magala ameomba ushirikiano kwa viongozi wa Chama pale ambapo wataona haendi sawa waweze kumkumbusha ili ilani izidi kutekelezwa.
Juni 15, 2024.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.