Mkuu wa Nkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiiangalia moja ya simu zilizotolewa na na GIZ kwa ajili ya kuandikisha wanachama wa Mfumo wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amepokea simu za mkononi 836 zenye thamani ya shilingi milioni mia moja sitini na saba na laki mbili kwa ajili ya kusajili wanachama wa mfuko wa Afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF Iliyoboreshwa). Simu hizo zimetolewa na Benki ya watu wa Ujerumani kupitia shirika la GIZ.
Akizungumzia msaada huo Mhe. Byakanwa ameshukuru wafadhili hao na kuwataka Idara ya afya kuhakikisha wanawafikia wananchi ndani ya wakati. Amesema lengo la mkoa ni kuhakikisha wanasajili kaya 360,000.
“Nitowe wito kwa wataalamu walioandaliwa kusajili wananchi kuhakikisha lengo linafikiwa kwa wakati. Aidha kila mwezi Mganga Mkuu wa Mkoa uhakikishe unaleta taarifa ya idadi ya kaya zilizosajiliwa”. Amesema Byakanwa
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuchangamkia fursa ya Bima ya afya ambayo inapatikana kwa gharama ndogo ya shilingi 30,000 kwa kaya.
Kwa upande wake Mshauri wa GIZ Mtwara, Paul Gogo ameshukuru ushirikiano anaoupata mkoani Mtwara. Amesema GIZ wana lengo la kuhakikisha jamii inapata afya njema na kwamba ongezeko la Simu 836 kutoka simu 30 walizozitoa hapo awali itasaidia kazi kufanyika kwa haraka zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.