Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa akimvalisha medali Maalumu Mkuu wa shule ya Sekondari Tandahimba Moses Mathias kwa kuwezesha shule kuwa ya kwanza kimkoa katika matokeo ya kidato cha sita kitaifa 2018.
Umoja na mshikamano kati ya walimu, wanafunzi, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa Elimu umetajwa kuwa sababu kuu ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita mkoani Mtwara. Umoja huo umewaimarisha na kuwatia moyo walimu na wanafunzi katika kutatua changamoto mbalimbali za kielimu hatimaye kuufanya mkoa wa Mtwara kuwa wa Kwanza katika mitihani ya kidato cha sita kitaifa mwaka 2018.
Hayo yamesemwa leo na walimu wa shule mbalimbali za kidato cha tano na sita mkoani Mtwara wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa kwa lengo la kuwapongeza walimu hao.
pata maelezo kwa undani pamoja na picha za tukio kwa kubonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.