Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amefanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa mtoto kutoka Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) nchini Tanzania Bi.Miranda Armstrong leo tarehe 02 Juni 2025 ambaye ameeleza lengo la kufika mkoani hapa ni kuona jitihada mbalimbali za kubaini, kuzuia na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.
Katika mazungumzo yao, CPA. Bahati ameishukuru UNICEF kwa mchango wake katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya na elimu.
Bi. Miranda alieleza kuwa UNICEF inashirikiana vema na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anasajiliwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kujenga uelewa kwa wananchi kuwa usajili huo ni bure.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.