Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema, bado Taifa halijafanya jitihada za kutosha kuwaanda wanamichezo katika kushiriki medani za kimataifa kutokana na kutoimarisha msingi wa michezo kutoka ngazi ya shule za awali.
Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo, hapa Mkoani Mtwara kwenye uzinduzi wa maishando ya kitaifa ya michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA).
Amesema yapo malalamiko mengi kuhusu wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri katika medani za kimataifa, Viongozi na wadau wengine wa michezo wanapaswa kukaa chini na kujiuliza kama wanawaandaa vyema wanamichezo hao na kisha kufanya jitihada za kukuza na kuendeleza vipaji ili waweze kuchangia kwenye uimara wa michezo.
Aidha Waziri Mkuu ameziagiza, Wizara na Mamlaka zote zinazosimamia maendeleo ya sanaa na michezo ziwajibike kikamilifu kuhakikisha watafuta mbinu za kuboresha michezo hapa nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, utamaduni sanaa na michezo Innocent Bashungwa amesema Ili kuwa na uendelevu wa vipaji vinavyovumbuliwa katika maishando ya kitaifa ya michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari, Wizara hiyo inatarajia kuanzisha kituo maalumu cha kuendeleza michezo katika chuo cha maendeleo ya michezo Malya Mkoani Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.