WATU 15 wamekamatwa Mkoani Mtwara kwa tuhuma za kuuza viuatilifu feki vya salpha na vya maji ambavyo vinavyotumika kudhibiti magonjwa ya zao la korosho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amewaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa watu hao wamekatwa na viuatilifu vya salpha tani 84.3 na vya maji lita 292 ambavyo vimeisha muda wake.
“Watu hao walikamatwa katika zoezi lilofanywa na jeshi la polisi mkaoni hapa baada ya kupata taarifa za awali za uwepo wa viuatilifu feki katika baadhi ya maduka maeneo mbalimbali Mtwara,” amesema.
Kufuatia hatua hiyo, Gaguti, ameliagiza jeshi la polisi kukamilisha taratibu za kipolisi na watuhumiwa waweze kufikishwa haraka kwenye vyombo vya sheria.
Pia ameagiza kufungwa kwa maduka pamoja na maghala ambayo yalihusika katika hujuma hiyo ya kuuza na kuhifadhi viuatilifu ambavyo vimeisha mda wake mpaka pale kesi ya msingi itakapokamilika.
Pia Gaguti amewaomba wananchi, pamoja na wakulima kuwa waangalifu na kufuatilia kuhakikisha ubora wa viuatilifu na madawa mengine wayanyotumia katika kudhibiti magonjwa ya korosho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.