Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 07 Februari 2025 amezindua mkataba wa baraza la wafanyakazi huku akiwasisitiza watumishi kuzingatia haki na wajibu wao.
Kanali Sawala ameeleza kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo pekee kinachounganisha menejimenti na watumishi ili kujadili mambo mbalimbali ya taasisi pamoja na kutatua migogoro kwa lengo la kuleta maendeleo ya taasisi na mkoa.
“Viongozi mpende kuwaunganisha wafanyakazi walio chini yenu, muwe kimbilio lao pindi wapatapo changamoto; muwe baraka kwao na si balaa.” Alieleza Kanali Sawala.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi hao kujiendeleza kitaaluma ili kuzidi kufanya kazi kiufanisi na kuleta matokeo chanya.
Kwa upande wake Mwenyeki wa Baraza hilo la wafanyakazi ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amesisitiza upendo na ushirikiano miongoni mwa watumishi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.