Viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) wametakiwa kutotumika kisiasa na badala yake kufanya kazi kwa weledi kwa lengo la kuwasaidia wakulima.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala wakati wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Mtwara ambapo pia amewataka Viongozi wote wa AMCOS na Vyama Vikuu vya Ushirika MAMCU na TANECU kuwatumikia wanachama ambao ndio wakulima kwa uaminifu,uadilifu pamoja na kuwalipa stahiki zao kwa wakati.
Amevipongeza vyama vya ushirika Mamcu na Tanecu kwa mafanikio makubwa waliyoyapata kwa kuendelea kusimamai mauzo ya mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani pamoja na kununua shamba lenye hekari 1500 kwaajili kulima mazao mbalimbali kwa upande wa Mamcu na Tanecu kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua korosho na kutoa ajira kwa maafisa ugani ili kuwa karibu na wakulima waweze kupata kero haraka kupitia maafisa ugani hao.
"Niwapongeze sana wana Ushirika kwa kazi nzuri mnayoifanya wote Mamcu na Tanecu,tumeona Mamcu mmenunua shamba hekari zisizo pungua 1500 na mmeshalima hekari 500 mnahitaji pongezi najua mtaweka jitihada ya kulima zaidi kipindi kijacho na nitakuwa nione ufuta mmepata kiasi gani,mbaazi na korosho zitakapoanza kuvunwa"
"Vilevile Tanecu mmejenga ukuta kwenye ghara lenu pale Tandahimba,mmejenga kongani me naita kongani mana hamtaishia tu kujenga kiwanda,lakini pia mnaendelea kurudisha kwa jamii maeneo mbalimbali hii yote ni kurudisha kile ambacho kinapatikana kwa wananchi wetu."Amesema Sawala
Aidha wale wote ambao wamepata elimu juu ya utumiaji wa mfumo mpya wa mauzo ya mazao unaojulikana kama TMX kutoa elimu kwa wanachama na wakulima ili waweze kujua mfumo huo unavyofanya kazi ili kuepusha taharuki.
Na amewataka viongozi kusimamia vizuri ugawaji wa pembejeo na kufanya kazi kwa uaminifu ili kuongeza uazalishaji wa zao la korosho pia amewaagiza bodi ya korosho kutoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa juu ya ugawaji wa pembejeo kilasiku.
"Naombeni kwa namna mlivyoahidi kufanya kazi zenu kwa uaminifu nendeni mkafanye kazi hizo kwa weledi mkagawe pembejeo hizo,ni kitu kisichoingia akilini pembejeo zipo ghalani alafu watu hawapei watu wa vyama vikuu viongozi mko hapa pembejeo zipo magharani alafu wakulima hawapewi mimi nitachukulia watu wanasababu binafsi ambazo hatutokubali,Bodi ya korosho na wakuu wa wilaya nitataka nipate taarifa kila siku jioni nipate taarifa ya hali ya ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wetu kila eneo."Amesema Sawala
Nae Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) Karim Chipola, amesema kuwa vyama hivyo wamepanga kuongeza uzalishaji wa zao la korosho,mbaazi na ufuta kwa kuanza kuchukua hatua ya kuanzisha mashamba makubwa ya korosho na ufuta na kuboresha huduma za kiugani kwa wakulima.
Pia amesema ushirika kwa pamoja wamejipanga kutatua changamoto ya kukosekana kwa wanunuzi kwenye mnada hivyo wamejipanga kusafirisha maafisa masoko kwenda nje ya nchi ili kuangalia masoko ya mazao ya ufuta,mbaazi na korosho ili kukabiliana na changamoto za kwenye minada.
Juni 20, 2024.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.