Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri, wataalamu wa afya na viongozi wa ngazi zote kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya Surua, Rubella na Polio. Agizo hilo limetolewa leo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda aliyemwakilisha katika uzinduzi wa kampeni hiyo zoezi lililofanyika katika Kituo cha Afya Likombe.
Amesema mkoa unajivunia mafanikio ya kutopata mgonjwa hata mmoja wa maradhi hayo tangu mwaka 2014 ilipotolewa chanjo hiyo.
“Mmesikia hapa, mkoa wetu wa Mtwara unahistoria, tangu kampeini ilipoanza mwaka 2014, hakuna mgonjwa wa surua, Rubella wala polio aliyeripotiwa. haya ni mafanikio makubwa sana.”
Amesema mkoa unatarajiwa kutoa chanjo ya surua na Rubella kwa watoto 161,241, na watoto 98,196 watapatiwa chanjo ya polio.
Kampeni hii iliyozinduliwa leo itaendelea hadi Oktoba 21, 2019 ikiwa na kaulimbiu ya ‘CHANJO NI KINGA, KWA PAMOJA TUWAKINGE’.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.