Vyama vikuu vya Ushirika mkoani Mtwara vimekabidhi hundi zenye thamani ya Tsh. Milioni 203 na mifuko 700 ya saruji yenye thamani ya Tsh. Milioni 13 kwa ajili ya kuinua shughuli za maendeleo katika sekta za Afya, Elimu na Maji.
Hundi hizo zimepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed katika ukumbi wa Boma, ofisi za Mkuu wa mkoa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Hundi hizo Meneja wa Tanecu, Ndg. Mohamed Nassoro amesema dhumuni kubwa la vyama vya ushirika ni kuona jamii ikinufaika na kuendelea kwani ndio jukumu lao kuu kupeleka maendeleo katika jamii.
Vyama hivo vya Ushirika vimemshukuru mkuu wa mkoa wa Mtwara kwa niaba ya viongozi wote wa mkoa, kwa ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwao kwani umesaidia kupunguza changamoto katika vikundi vingi vya ushirika.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Mtwara alipata wasaa wa kutoa neno la shukrani mara baada ya kupokea hundi hizo.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.