Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi maalum), Mhe. Kapt. George Huruma Mkuchika amevitaka vyama vya Ushirika kuhakikisha mazao yanayozalishwa kanda ya kusini yanaingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani (TMX) ili kumhakikishia soko mkulima.
Mhe. Mkuchika ametoa rai hiyo leo tarehe 06 Agosti 2025 alipoungana na washiriki wa maonesho ya nanenane kanda ya kusini katika hamasa ya matumizi ya mbegu asili na vyakula vya asili.
“Mikorosho ya siku hizi usipopuliza dawa unakosa korosho, tunamshukuru Rais Samia kwa kutupa pembejeo bure, tumeweza kuongeza uzalishaji wa korosho. Niwasihi wakulima wenzangu tupalilie mashamba kwa wakati, tusipalilie kwa moto.”Alieleza Mhe. Mkuchika
Aidha, Waziri Mkuchika ameitaka jamii kuhakikisha wanakula vyakula visivyo hatarishi kwa afya na badala yake amewasihi kupenda kula vyakula vya asili vyenye lishe bora ili kuweza kustawisha jamii.
“Tumekuwa tukiwashirikisha wakulima katika tafiti zetu, majibu anayotoa mkulima sisi tunaboresha na kutengeneza mbegu bora zinazompa mkulima tija.” Alieleza Dkt. John Tenga, Kaimu Mkurugenzi wa TARI-Naliendele.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.