Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 10 Februari 2025 ameongoza kikao cha wadau wa maendeleo kujadili namna ya kusaidia walioathiriwa na mvua mkubwa zilizonyesha mapema mwezi huu.
“Sote tunafahamu mvua kubwa zilizonyesha mkoani kwetu na madhara yaliyotokea, ndugu zetu wana Mtwara hawana chakula, wengine hawana pa kuishi kufuatia nyumba zao kubomoka. Niwaombe kwa chochote tulichojaaliwa na Mwenyezi Mungu tuwashike mkono kuwasaidia wakati huu mgumu kwao.” Alieleza Mhe. Mwaipaya
Mratibu wa maafa mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Kyaruzi alieleza kuwa kata 15 za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani zimeathiriwa na mvua ambapo nyumba 746 zimeingiliwa maji, 145 zimebomoka na watu 205 wamekosa makazi.
Bw. Kyaruzi alieleza jitihada zilizofanywa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwemo kutenga maeneo ya kuwahifadhi watu endapo mvua zitaendelea. Pia ameeleza namna mamlaka mbalimbali zinavyoshughulikia uboreshaji wa miundombinu ili shughuli za kijamii na kiuchumi zisikwame.
Wadau hao wa maendeleo kwa pamoja wametuma salam za pole kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara pia wamepongeza jitihada zinazoendelea kusaidia waathirika wa mvua na kuahidi kuunga mkono kutoa misaada ya kibinadamu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.