Mpango wa kuhamasisha elimu mkoani Mtwara kwa kuwatambua walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo umepongezwa na wadau wa Elimu hapa nchini. Mpango huo ulioanzishwa Na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa unahusisha kuweka vibao vya kumbukumbu ya majina ya Walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwa kila mwaka.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kutembelea maeneo yanayotekeleza mradi wa Tusome pamoja mkoani Mtwara, iliyofanywa na wadau wa mradi huo kutoka mikoa inayoutekeleza hapa nchini, Mshauri wa Elimu mkoa wa Lindi kupitia shirika lisilo la kiserikali la ‘Education Quality Improvement Program’ (EQUIP-T) Digner Peter amesema mpango huo ni mzuri na unatoa hamasa kwa wanafunzi na walimu kufanya jitihada zaidi.
“Kilichonifurahisha sana ni vile vibao nilivyoviona hapo shule ya Msingi Mihambwe. Niliona vibao ambavyo vinamtangaza mwalimu bora na mwanafunzi bora... Sisi tunaweza kuwa tunakiona kama ni kitu kidogo, Jamani hicho siyo kitu kidogo kwa wenzetu wazungu wangekikuza hicho. Mtu kuacha historia nzuri mahari siyo kitu kidogo. Hata kwa hela zangu nitatafuta shule hata moja Nikakifanye”. Ameeleza Digner.
Mapema mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gerasius Byakanwa aliagiza halmashauri zote kuhakikisha zinatengeneza mazingira ya kujenga hamasa ikiwa ni pamoja na kuweka vibao vya kuwatambua mabingwa wa mwaka husika.
Pia wahakikishe Mitaala inamalizika mapema ili kuwapa wanafunzi muda wa kutosha kufanya mitihani ya kujipima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.