Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewataka wanamtwara wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma katika ngazi zote kujitokeza kutumia fursa za Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkoani humo tukio linalotarajiwa kufanyika April, 1 , 2023.
Kanali Abbas ametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Mtwara ambapo ametoa taarifa rasmi kwa umma kutambulisha tukio la Uzinduzi wa mwenge kitaifa na kusisitiza kuwa tayari Mkoa umejipanga kuhakikisha malengo ya shughuli hiyo yanafikiwa.
Kanali Abbas amesema kuwa tayari Mkoa umeandaa ratiba yake ya matukio yatakayojiri kuanzia mwishoni mwa mwezi Februari hadi hadi April, 01, 2023 ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Uzinduzi wa Mwenge Mkoani Mtwara.
Ndugu Wanahabari, napenda kuchukua fursa hii kuwaarifu kuwa Jumamosi ijayo ya tarehe 18/02/2023 tunazindua rasmi kampeni zetu za Uzinduzi wa Mwenge Kimkoa ambapo tutaanza na tukio la matembezi ya hisani.
" Ndugu waandishi wa Habari siku hiyo ya Jumamosi tutafanya matembezi kuanzia mashujaa kupitia soko la zamani na Skoya hadi Uwanja wa Nangwanda ambako pia kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo burudani" alisema Kanali Abbas.
Kanali Abbas pia amesisitiza umuhimu wa wadau na wafanyabiashara kujitokeza kushuhudia tukio hilo la matembezi ya hisani kwani litawapa dira ya namna ya kujiandaa kulikabili tukio hilo kubwa la Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Aprili 2.
Mwenge wa uhuru utazinduliwa Mkoani Mtwara ambapo zaidi ya wageni 1000 Kutoka Mikoa mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameviomba vyombo vya habari kuwahasisha wanamtwara na watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika tukio hilo la Kihistoria ambalo limebeba heshima ya Mkoa na taifa kwa ujumla.
" Mkoa wetu umepewa heshima kubwa ya Kuzindua mwenge wa Uhuru kitaifa, na sisi kama Mkoa tumeamua kulipa umuhimu wa kipekee tukio hili, ndio maana tumeandaa shughuli mbalimbali zitakazoendana na ratiba ya matukio ya kitaifa na kimkoa kwa ujumla" alisisitiza Kanali Abbas.
Aidha Kanali Abbas ameyataja matukio mengine yatakayojiri kati ya Machi na Aprili 2023 ni pamoja na makongamano na maonesho ya kazi za wanawake katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani, maonyesho ya bidhaa mbalimbali, shughuli za kijamii katika halmashauri pamoja na midahalo na maonyesho katika juma la Elimu.
Hivyo ninawaomba ndugu waandishi mtumie kalamu na kamera zenu kuwahamasisha wananchi kushiriki katika matukio yote kuelekea siku ya uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru.

MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.