Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka wananchi Mkoani Mtwara kujiandaa kutoa maoni yao ya kuandaa Dira ya tatu ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050.
Kanali Sawala amesema Serikali ipo katika utaratibu wa kupokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusiana na dira ya maendeleo ya Miaka mingine 25 ijayo.
Kanali Sawala amesema kuna wataalamu watakuja Mkoani humu kukusanya maoni na matarajio ya wananchi namna ambavyo wanataka Tanzania iwe kwa miaka 25 ijayo.
"Wataalamu watakapofika wananchi muwape maoni yenu mnataka Tanzania ya aina gani au iweje kwenye Mkoa wa Mtwara kwenye sekta mbalimbali kama vile maji, Afya, Huduma za jamii, mazingira na nyingine, " amesema.
Dira ya Kwanza nchini ilianza mwaka 2005-2019 , ya pili mwaka 2020-2025 na ya tatu ni mwaka 2025-2050.
Dira ni mwongozo au taa ya kuonyesha Taifa (nchi) ni nini cha kufanya kwa mahali gani, Kwa jinsi gani ,na kwa wakati gani na kwa watu gani.
Aprili 29, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.