Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa ametoa wito kwa Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wa kutengeneza barakoa (Mask) watengeneze kwa wingi. Wito huo ameutoa leo Aprili 17, 2020 wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maradhi ya COVID-19 kutoka kwa kampuni ya Beijing Construction and Engineering Group CO. LTD inayoshughulika na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Amesema mahitaji ya vifaa hivyo kwa sasa ni makubwa hasa kwa watoa huduma na watu wote ambao kila siku wanafanya kazi ya kukutana na watu. Aidha, amesisisitiza jamii kuendelea kujikinga na ugonjwa huo kwa kuzingatia tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa huku akiwasisitiza wageni wanaotembelea ofisini kwake kuhakikisha wanavaa barakoa.
“..na mimi kama Mkuu wa Mkoa, tutakapoanza wiki inayofuata, hakuna mtu atakayefika kwenye ofisi yangu bila kuvaa Mask. kuanzia jumatatu tarehe 20, kila mtu atakayefika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa atapaswa kuwa amevaa Mask.” Amesema Byakanwa.
Naye Meneja wa kampuni ya Beijing Construction Cui Rui Tao ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa hatua inazochukua dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Amesema wameona umuhimu wa kusaidia jitihada hizo kwa kutoa msaada wa Barakoa elfu moja, galoni 10 za lita tanotano Pamoja na vitakasa mikono.
kuangalia video Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.