Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bi. Nanjiva Nzunda wamekabidhi misaada yenye thamani ya Shilingi 1,048,000/= kwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara ikiwa ni kwaajili ya kusaidia walioathiwa na mvua zilizonyesha mapema mwezi huu.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Nanjiva Nzunda ambae pia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa ameeleza namna watumishi walivyoguswa na kuamua kuchanga fedha zilizowezesha kununua mahitaji hayo ya kibinadamu kwaajili ya kuwasaidia walioathiriwa na mvua.
Misaada iliyokabidhiwa ni pamoja na mafuta, unga, mchele, maharage, sukari, sabuni na mahindi.
Kwa upande wake Mhe. Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amewashukuru watumishi hao kwa moyo wa upendo waliouonesha.
Mhe. Mwaipaya ametoa rai kwa watu na makampuni kuzidi kujitokeza kusaidia walioathiriwa na mvua.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.