Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajia kutembelea mikoa ya Mtwara na Lindi kesho. Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Gasper Byakanwa wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisni kwake amesema Mheshimiwa Majaliwa ataanza ziara kwa kuzindua mradi wa kuiunganisha Lindi na Mtwara katika gridi ya Taifa ya umeme. Zoezi hilo litafanyika katika kijiji cha Mahumbika huko Lindi.
Baada ya zoezi hilo ataenda Bandari ya Mtwara kujionea miundombinu ya uingizaji wa mafuta kupitia Bandari hiyo kisha kuzindua upanuzi wa kituo cha kufua umeme cha Mtwara, umeme ambao kwa sasa unatumiwa na mikoa ya Lindi na Mtwara. Amesema upanuzi unahusisha ongezeko la Mashine mbili zilizoingia hivi majuzi za kufua umeme wa megawati 4. Kwa sasa kituo hicho kina mashine nane ambazo zikifanya kazi zote huzalisha megawati mbili mbili na kufanya jumla ya megawat 18.
Sambamba na uzinduzi Mheshimiwa Majaliwa atafanya mkutano wa Hadhara katika eneo hilo.
Mheshimiwa Byakanwa amewataka wananchi wote wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kujitokeza kwa wingi kumlaki na kusikiliza jinsi serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza ahadi zake.,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.