Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoa pongezi kwa hospitali ya wilaya ya Tandahimba kwa kufunga mfumo wa kielektloniki wa kurekodi mahudhurio ya watumishi katika hospitali hiyo. Pongezi hizo amezitoa leo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Tandahimba
Amesema hiyo ni njia sahihi katika kurahisisha utendaji kazi na ina rahisisha ufuatiliaji wa mahudhurio kwa watumishi.
Aidha Mheshimiwa Waziri ameagiza Hospitali zote za Wilaya na Mikoa kuhakikisha zinafunga mfumo huo ndani ya siku 60.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Said Msomoka ameshukuru serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi. Amesema wameamua kufunga mashine hizo ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia.
Amesema matumizi ya mifumo hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mahudhurio ya watumishi na kurahisisha utoaji wa stahiki za mtumishi ikiwemo malipo ya ziada kwa watumishi wanaofanya kazi nje ya muda wa kawaida wa kazi.
“Badala ya utaratibu wa zamani wa kutambua stahili ya mtumishi katika malipo ya ziada hii inasaidia sana kwani mfumo unatoa taarifa ya muda wote ambao mtumishi alikuwepo kazini na hivyo kuondoa malalamiko ya watumishi”. Amesema Msomoka
Amesema maeneo mengine walipofunga ni makao makuu ya halmashauri, Kituo cha Afya Mahuta na Kituo cha Afya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.