Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed Mapema leo hii Feb 26, 2024 ameanza ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo katika Halmashauri za Mkoa wa Mtwara Ambapo ameanza na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Kanali Ahmed amesaini kitabu na kupata maelezo mafupi ya utekelezaji wa miradi ya Halmashauri katika ofisi kuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na baada ya hapo amekagua ujenzi wa madarasa 4 na Matundu 12 ya vyoo katika shule ya Msingi Naliendele. Pia Kanali Ahmed ametembelea na kukagua Ujenzi wa Barabara kiwango cha lami kata ya likombe yenye kilomita 1. pamoja na hayo akamalizia kukagua ujenzi wa kisima cha kuvunia maji ya mvua kata ya majengo (TASAF) na kuongea pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Mkuu wa Mkoa afurahishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo pamoja na kutoa maelekezo machache kwa watendaji kwa kuboresha zaidi miradi hiyo.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.