ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA SEKTA YA ELIMU
Posted on: June 10th, 2025
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala Leo juni 10, 2025 ameanza kukagua miradi ya maendeleo Katika sekta ya Elimu ambapo amekagua miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3.2
Siku ya kwanza ya ziara yake Katika halmashari za Mkoa wa Mtwara Kanali Sawala akiambatana na kamati ya usalama Mkoa wamekagua miradi ya ujenzi wa shule za Sekondari Katika halmashari za wilaya za Mtwara, Tandahimba, Newala na Mji Namyamba.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya sekondari Hinju Katika halmashari ya mji Namyamba , Kanali Sawala amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwekeza sekta ya elimu ili kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kupata elimu.
"Ndugu wananchi mliofika kufuatilia maendeleo ya mradi huu, nichukue fursa hii kuwapongeza Kwa uzalendo wenu Kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utekelezaji wa mradi huu, Mhe. Rais ameniagiza niwape salamu zake anasema mtakapokamilisha vizuri mradi huu, atawaletea fedha nyingine nyingi za miradi" alisisitiza Kanali Sawala .
Akiwa Katika halmashari ya wilaya Tandahimba Kanali Sawala amekagua mradi shule ya amali iliyojengwa Katika kijiji cha Mkwedu Kwa gharama ya shilingi milioni 560.6 mradi ambao umetekelezwa Kwa asilimia 90 mpaka kufikia sasa huku akionyesha kuridhishwa na kiwango cha ubora katika hatua za utekelezaji wake.
Siku ya kwanza ya ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo ilihitimishwa Kwa zoezi la ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Mcholi katika Halmashauri ya Mji Newala ambapo Kanali Sawala amesema serikali itaendelea kufuatilia Kwa Karibu miradi yote ya Maendeleo Ili kuhakikisha inaendana na thamani ya fedha iliyotumika.
Jumla ya miradi 8 ya Ujenzi wa Miundombinu ya elimu katika halmashauri 4 za Mkoa wa Mtwara imetembelewa katika siku ya kwanza ya ziara hiyo.