Kutokana na kugundulika kwa gesi asilia, viwanda vya mbolea na methanol vinatarajiwa kujengwa katika eneo la bandari lililotengwa kwa ajili ya ukanda wa viwanda wa bandari. Kwa sasa Mkoa umeshapata mwekezaji kampuni ya HELM kutoka Ujerumani ambayo Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding) kati ya Kampuni ya HELM na Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Mtwara ilisainiwa tarehe 21/07/2014. Kwa sasa taratibu mbalimbali zinakamilishwa ili kuwezesha kazi ya upembuzi yakinifu kuanza. Aidha, baada ya kampuni ya HELM kuanza uzalishaji makubaliano ni kuwa itaundwa kampuni ya ubia hapa nchini kati ya RCC na HELM ambayo itahusika na umiliki, ujenzi na uendeshaji wa viwanda ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa bidhaa zitakazotokana na viwanda hivyo.
Kwa maelezo zaidi yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakati wa ziara yake Agosti 2016 mkoani Mtwara Bonyeza Hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.