Ziara ya Kujifunza Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji Biashara ya Hewa ya Ukaa Inayojumuisha Wataalamu Kutoka Halmashauri za Wilaya na Wataalamu Kutoka RS Mtwara Wakiongozwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri Imekamilika jioni ya Leo Mkoani Katavi.
Kesho Ujumbe huo Inaondoka Kuelekea Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma Kujifunza Masuala Mbalimbali yanayohusiana na Uzalishaji wa Chumvi na Mwenendo wa Biashara yake.
Februari 17, 2024.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Februali 2019 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aliagiza wakuu wa wilaya wote mkoani Mtwara kuhamasisha kilimo cha ufuta katika maeneo yao ili kuondokana na kutegemea zao la korosho pekee.
Agizo hilo lilienda sambamba na kuzitaka halmashauri kuanzisha mashamba darasa ya ufuta ambayo yaliwekwa chini ya usimamzi wa wataalamu wa Taasisi ya Utafitiwa Kilimo Tanzania Kituo cha Naliendele (TARI-Naliendele)
Halmashauri ziliitikia wito huo kwa kuanzisha mashamba hayo ambayo sasa yanendelea vizuri.
Pia walisimamia wananchi kuanzisha mashamba ya mtu mmoja mmoja, mashamba ya familia na mashamba ya vikundi vya vijana. Baadhi ya mbinu zilizotumika ni pamoja na kuwagawia wakulima mbegu kwa matarajio ya kuwa baada ya kuvuma watarudisha kiasi kilekile walichopewa ili serikali ya eneo husika ikigawe kwa wakulima wengine.
Wakulima walioitikia wito huo wanaanza kuiona dunia inayowezekana kupitia kilimo cha ufuta. Bwala Udede ni mmoja wa wakulima ambaye anataraji kupata zaidi ya milioni kumi ndani miezi miwili ijayo. Msikilize hapo kwenye video hiyo ya dakika mbili tu.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.