Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa ameagiza walimu wote mkoani Mtwara waliopewa nyumba za kuishi kuingia mikataba na Halmashauri kwa ajili ya utunzaji wa nyumba hizo.
Agizo hilo amelitoa jana wakati akikagua nyumba za walimu wa shule ya msingi Lulindi 1 iliyoko kijiji cha Muungano kata ya Lulindi Wilayani Masasi mara baada ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kimkoa lililofanyika kijijini hapo.
Mheshimiwa Byakanwa amesema hatavumilia mwalimu anayepewa nyumba bure kushindwa kuitunza. Anasema ni bora nyumba hiyo akapewa mwalimu mwingine mwenye moyo wa kuitunza kuliko Mwalimu anayesubiri serikali imfanyie kila kitu.
Amesema serikali inaendelea na mipango ya kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuleta vifaa vya maabara kwa shule za sekondari kote nchini
Amerishishwa na hali ya ukusanyaji wa fedha za Ndani na mshikamano walio nao hapo Tandahimba.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.