Mkuu Wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amefunga mwaka 2017 kwa kupokea mikakati ya utendaji kazi toka kwa wakuu wa Idara na vitengo wa Ofisi Yake. Katika Kikao hicho kilichoafanyika leo Ofisi kwake Mheshimiwa Byakanwa amepokea taarifa za mafanikio na mikakati ya mwaka unaofuata kwa kila Mkuu wa Seksheni na Kitengo na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mheshimiwa Byakanwa ambaye alichaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huu hivi karibuni amesema anahitaji kuona Ofisi yake inakuwa na umoja na wote wanafanya kazi kwa ushirikiano.
Awali wakiwasilisha taarifa hizo wakuu wa Idara wameahidi kufanya kazi katika miongozo na maagizo anayoyatoa kama kiongozi wao Mkuu. Aidha wamesema ziko changamoto nyinig lakini zote zina majibu yake ambayo yanawapa matumaini ya kuleta mabadiliko katika idara.
RC Mtwara ametoa msaada wa chakula kwa wasiojiweza
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema vijiji vyote vya mkoa wa Mtwara utafikiwa na umeme katika awamu mbili zinazofuata.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.