Msanii wa Bongo Fleva Haromonize ametua Mjini Mtwara Tayari kuungana na wakazi wa mji wa Masasi kwa ajili ya kuutangaza utalii wa mji huo kupitia mlima Mkomaindo. Harmonize ambaye ametua na kundi la wasanii wenzake amesema lengo lake ni kuhakikisha sanaa ya kusini inainuka na hivyo kufikia ndoto yake ya kuhakikisha analipa fadhila kwa heshima aliyopewa na watu wa Kusini.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Japhet Hasunga amesema malipo ya wakulima wa korosho yameanza leo na kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya uhakiki ambao umekamilika kwa vyama vya Msingi 35 vikiwa vikiwa ni katika mkoa wa Mtwara.
Amesema bao uhakiki unaendelea na kwamba ndani ya wiki mbili watakuwa wamekamilisha na hivyo kila mkulima aliyefiksiha korosho yake sokoni kulipwa fedha yake.
Mheshimiwa waziri ameyasema hayo leo wakati wa kikao chake na waandishi wa habari klilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Boma uliko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa MTwara.
Ametahadhalisha baadhi ya wakulima ambao baada ya kuona serikali inanunua korosho kwa bei nzuri wameanza kuingiza korosho ya daraja la chini ambayo ilibaki kwenye misimu iliyopita. amesema wako makini na watahakikisha jambo hilo halijitokezi.
AIdha mheshimiwa Waziri amesema fedha hizo zitalipwa moja kwa mmoja wka wakulima badala ya kuzipitisha kwenye vyama vya msingi ili kuhakikisha fedha inamfikia mkulima wka haraka zaidi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Oktoba, 2018 amekutana na wanunuzi wa zao la korosho na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya zao la korosho kufuatia kuwepo kwa mvutano wa bei ya zao hilo kati ya wanunuzi na wakulima.
Rais Magufuli amekutana na wanunuzi hao katika mkutano wa majadiliano uliokuwa ukiendelea kati ya wanunuzi wa korosho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.