Umaarufu wa mkoa wa Mtwara katika kula chakula aina ya panya ni fursa mojawapoa ya kuvutia utalii mkoani hapa. Akizungumza katika kipindi cha safiri nasi kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema hilo ni mojawapo ya malengo yake kuhakikisha fursa mbalimbali za mkoa wa Mtwara ikiwemo ulaji wa panya unatumika kama kivutio cha utalii.aidha yeye mwenyewe atakuwa wa kwanza kushiriki chakula hicho kinachotajwa kuwa kitamu zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria Meneja Wa Chama cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU), Afisa Ushirika wilaya ya Tandahimba, Makatibu wa Vyama kadhaa vya msingi na baadhi ya wananchi ambao wameshiriki katika ufisadi wa kutisha katika kilimo cha korosho mkoani hapa.
Mheshimiwa Byakanwa amechukua uamuzi huo baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi wa madai ya malipo ya fedha za wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2016/20117 na 2017/2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambayo iliundwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Sebastian Muungano Walyuba.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa ameagiza walimu wote mkoani Mtwara waliopewa nyumba za kuishi kuingia mikataba na Halmashauri kwa ajili ya utunzaji wa nyumba hizo.
Agizo hilo amelitoa jana wakati akikagua nyumba za walimu wa shule ya msingi Lulindi 1 iliyoko kijiji cha Muungano kata ya Lulindi Wilayani Masasi mara baada ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kimkoa lililofanyika kijijini hapo.
Mheshimiwa Byakanwa amesema hatavumilia mwalimu anayepewa nyumba bure kushindwa kuitunza. Anasema ni bora nyumba hiyo akapewa mwalimu mwingine mwenye moyo wa kuitunza kuliko Mwalimu anayesubiri serikali imfanyie kila kitu.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.